34. Wakristo Furahini

Sauti na wimbo: freut euch, ihr lieben Christen.
L.B.W. 87. N.K. 32
Mtunga Sauti: L. Shroeter, 1587
Asili: 1540


1. Wakristo furahini,
furahini sana!
Mwaipigiwa leo
mbiu yenu njema!
Malaika wanaimba
huko juu mbinguni,
/: wanaimba vizuri
sauti ya kushangaa! ะ/


2. Hivi wanavyoimba:
Furahini nyote!
Acheni kuogopa,
tazameni nyote
kwani amezaliwa
Mwokozi wa pekee:
/: ni Bwana Yesu Kristo,
Mwana Mungu wetu:/


3. Shangilieni nyote
na kusikiliza.
Wapigieni nyote
mbiu na sauti kuu.
Mungu katupa sote
mtoto wa mbinguni,
/: kwa kutupenda sisi
amekuja kwetu. ะ/

Comments

Popular posts from this blog

17. Tuimbe na kusifu

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu