60.Ufalme wa Mungu
1. Ufalme wa Mungu
Uenee popote!
Nguvu yako iokoe
wakaao gizani.
Uondoe woga wote,
ukawape watu uzima,
Ufalme wa Mungu.
2. Ushinde upesi!
Uharibu ufalme
wa shetani duniani,
ndiye mfalme wa giza.
Nawe utamshinda yeye,
kwani una nguvu ya
Mungu.
Ushinde upesi!
3. U shujaa wa Mungu!
Kwa rehema ya Bwana
urudishe watu kwako,
wapendane kwa moyo,
wawe raia wako pote.
Ndipo utatukuzwa sana!
U shujaa wa Mungu!
4. Duniani popte
Jina lako livume
nguvu zako zisifiwe
na makabila yote,
uliowatengemaza,
mpaka utakapotawala
duniani popote!
5. Shikeni amri hii:
Tangazeni popote
kwa makabila yoyote
Neno lenye fuaraha,
wapate kuokolewa.
Yesu alivyotuagiza.
Shikeni amri hii!.
6. Sifuni rehema
ya kuokoa watu!
Tukimtumikia Bwana,
azibariki kazi zote za mikono yetu;
amani kuu iwe kwetu.
Sifuni rehema!
Comments
Post a Comment