58.Jina Moja ni Kubwa Sana


1. Jina moja ni kubwa sana:
Ni Jina lako Bwanangu!
Nasifu Jina hili lako,
Yesu Kristo u mwokozi.
Li tamu kwangu Jina hili,
Jina jingine silijui.



2. Naliandika Jina hili
rohoni mwangu kabisa.
Silisahua siku zote,
halifutiki moyoni.
Li tamu kwangu Jina hili,
Jina jingine sitafuti.


3. Jina hili ni jua langu
Lawaka ndani ya roho.
Lanipa na utengemano,
Lafuta makosa yote.
Li tamu kwangu Jina hili,
Jina jingine sifahamu.


4. Jina hili ni boma langu,
upanga wangu vitani,
ni ngao yangu na silaha,
la mshinda hata shetani.
Li tamu kwangu jina,
jina jingine silitaki.


5. Jina hili lanipa nguvu,
niweze kwenda kwa haki.
Ujuzi wote umo humo 
Katika jina la Yesu.
Li tamu kwangu Jina hili,
Jina jingine sitamani.


6. Eee Yesu, Jina lako ndilo 
furaha yangu nikifa.
Ni cheti cha kuingilia 
Mbinguni kwa Bwana
Mungu.
Ndipo nitalisifu sana,
Jina jingine silijui.



 

Comments

Popular posts from this blog

17. Tuimbe na kusifu

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu