57.Nani Mpenzi Wangu Mkuu?
1. Nani Mpezi wangu
Mkuu?
Nani ninayemsifu?
Nani ninayemjua?
Nani ninayempenda?
/:Ndiye Yesu
Mwokozi.:/
2. Nani ni mtegemee,
anipaye moyo mkuu?
Nani aondoaye,
makosa , shida zangu?
/:Ndiye Yesu Mwokozi.:/
3. Nani anayenipa,
Nguvu nyingi za roho?
Nani anifanyaye,
Mwenye haki kwa Mungu?
/:Ndiye Yesu
Mwokozi.:/
4. Nani mwenye faraja,
nikiona huzuni?
Nani atulizaye,
moyo wenye taabu?
/:Ndiye Yesu
Mwokozi.:/
5. Nani azishindaye,
Hata nguvu za kufa?
Nani anipeleke,
Baadaye kwake Mungu?
/:Ndiye Yesu
Mwokozi.:/
Comments
Post a Comment