56.Mmoja ni Mfalme
1. Mmoja ni mfalme shujaa,
Ni mshindaji!
Enyi adui, kimbieni tu!
Nawe sayuni uone furaha
ukapumzishe kabisa
moyo:
Uzima, utengamano,
furaha ndizo Mwokozi
atakazokupa.
2. Twende kuonja
maji ya uzima
tunayopewa
na Bwana Yesu
aliyesema
“Njooni kwangu nyote”
nitapumzisha mioyo
yenu.”
Nyweni, wapenzi,
katika kisima
chenye wokovu
wa wenye huzuni.
3. Mfalme wa mbingu
akuwapa
kilemba kizuri cha
urembo,
awawekea vitu vya milele,
heshima hiyo ni ya
kushinda.
Vumilieni taabu na shida:
Yesu mwenyewe
ni tuzo la vita.
4. Nguvu, ujuzi,
heshima na sifa
ni zake Mungu
na Mwana Wake.
Nami nataka kufika
mbinguni!
Nifunguliwe mafungo
yangu!
Mwenye upendo atanisikia.
Wenye uzima wanamsifu
Mungu.
Comments
Post a Comment