55. Mmoja ndiye tumpendaye
1. Mmoja ndiye tumpendaye
Aliyetoa mwili wake
Akikubali mateso
twakupa moyo Yetu
Mwokozi aliyetufia,
twapenda kuwa wako tu.
Bwana tukubali!
Ututengeneze sisi wako.
Nuru yako itung’aze
tusipotee gizani.
2. Sisi hatukukuita,
ila umetuita wewe,
huruma yako ni kubwa
Nguvu zetu hazitoshi,
kukufanyia kazi njema
usipotutia nguvu.
Shida yetu ni sisi
ndio ulegevu, uondoe;
nia zetu zigeuzwe
tufanaye kazi kwa bidii.
3. Yesu, wewe umesema:
“ Watenda kazi ni wachache
Kwenye mavuno ya bwana.”
Twaomba: Tutume nasi,
tualike wageni wengi,
Nyumba ya Bwana ijae.
Heri watu wale
uliochagua kuja kwako
kwenye raha na furaha
milele hata milele.
4. Uwahurumie watu
walio mbali na wokovu
wanaoshikwa na giza.
Hawajasikia bado.
Utume mwema wa wokovu
tunaopewa na Mungu.
Jua la uzima
liche hata kwako.
Njoo Mwokozi!
Tangulia! Twafuata,
Ukifungua mlango.
5. Tunataka kutangaza
Habari ya upendo wako,
Ya moyo wako wa kweli.
Tutawaonyesha watu
msalaba wako siku zote,
mpaka washindwe
mioyoni.
Kwani Neno lako
Lina nguvu kubwa
ya kushinda.
Comments
Post a Comment