54.Yesu u Nyota Kubwa
1. Yesu, u nyota kubwa,
itokayo kwa Yakobo,
Moyo wangu wapenda
kukutumikia leo.
Ukubali vipaji
niviletavyo mimi.
2. Ninaleta dhahabu,
Ndio kukutegemea,
Nalo ni paji lako,
Ulilonipa mwenyewe;
Nikushike kwa kweli
Hata majaribuni.
3. Nao uvumba wangu
ni maombi yangu mimi,
midomo na mioyo
Usikome kuyatoa.
uyakubali haya
kuwa uvumba mzuri.
4. Nayo majuto yangu
Ndiyo manemane yako;
Kwani hunipokea,
Nikikujutia kweli.
Nasema kwa furaha:
Watwaa matunzo yangu!
Comments
Post a Comment