51.Yesu ndiye kiongozi wangu


1. Yesu ndiye kiongozi 
       wangu,
      kumfuata Yeye ni furaha,
      ajuaye kuongoza vema,
      anilinda nisione shida,
      analeta raha moyoni.


2. Bwana Yesu akiniongoza,
Nitapita pori na misitu,
Nitavuka mito na bahari
Kwa furaha, kwani nina
        njia 
        ya kufika mjini kwa Mungu.


3. Nikilala Yesu anilinda
          anitunza Yeye siku zote.
          Hata nikifika njia panda,
          Nikiona shaka, aonyesha 
          njia ya kufika kwake.


4. Siku zote namfuata Yeye,
Sitaona kiu wala njaa;
anitunza kwa rehema 
nyingi:
nitaweka mikononi mwake
moyo wangu, auokoe.





Comments

Popular posts from this blog

17. Tuimbe na kusifu

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu