49.Nakutegemea Yesu
1. Nakutegemea Yesu,
Yesu peke yako tu.
Wewe u Mkombozi
wangu
unitulizaye.
Nakutegemea Yesu,
Kwani u Mkombozi
Ukinifia.
Ndipo nikakupenda sana,
wala sikuachi!
2. Wewe Mfalme
mkubwa sana
unaondoa dhambi.
Wanionea huruma,
Huna madanganyo.
Nakutegemea Yesu,…
3. Wewe umechunga
kondoo,
ukitanguliza mwanga.
Nakungoja mwongozaji,
nisipotee njia.
Nakutegemea Yesu,..
4. Wanichukulia mzigo,
sianguki majini.
Natambua wanipenda,
huniachi pekee.
Nakutegemea Yesu,….
5. Bwanangu umeniweka
ufalmeni ni kuzuri.
Nasifu damu yako
inayoniosha.
Nakutegemea Yesu,..
Comments
Post a Comment