48.Yesu Mponya tu Hapa


1. Yesu Mponya tu hapa,
moyo watulia,
mawazo yetu yote
uyavute kwako.
Mwanga wa Neno lako,
Utuangaze wote,
tuwe na mwangazo.


2. Kaa karibu nasi,
tunakutamani,
mfunzi wetu ni wewe,
sisi wanafunzi.
Nenolo lina nguvu,
litatufanya wapya,
laongoza vema.


3. Tuna furaha kubwa,
tunakungojea.
Wewe u mwamba wetu
tutegemeao.
Bwana tunakushika
mpaka tunapofika
Uzimani kwako.


4. Twataka utufunze
kuwa na upole.
Tufanane na wewe
Unyenyekeavyo.
Utimizavyo kazi,
Ulivyofanya bidii
Kuwa mpatanishi.


5. Nguvu ya Roho wako
ionyeshe kwetu,
Unavyomulika 
wanaopotea.
Kwa kinywa chako Yesu
Utushindie nasi,
tuwe wako kweli!




Comments

Popular posts from this blog

17. Tuimbe na kusifu

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu