47.Anza Siku Yako Hii
1. Anza siku yako hii
kwa jina la Yesu;
Mwombe akujalie,
usimame naye.
Kazi zako zote wee
atazibariki.
Na tena ulalapo,
atakuwa kwako.
2. Asubuhi mapema
Umwombe Mwokozi,
akusaidie Yee
shidani popote.
Atasimama kwako
Siku kuchwa pia,
na kumshinda
Shetani akikujaribu.
3. Yesu akiwa nawe,
waacha maadui,
usiogope hila
zao zote mbaya.
Umtegemee Yesu,
shika mkono wake;
mtegemee Mwokozi,
Yeye atashinda.
4. Mambo yangu na shida
ninakuwekea
kama unavyopenda,
zimalize zote.
Kazi yangu nianze
kwa jina la Yesu
nakuomba: njoo kwangu,
unisaidie!
Comments
Post a Comment