46.Twendeni Tumshukuru


1. Twendeni tumshukuru
Na kumwimbia Mungu,
Aliyetupa roho
Na nguvu mpaka leo.


2. Twaemda na kukua
Miaka yetu yote.
Hivyo mwaka kwa mwaka
Twafikia uzee.


3. Twaona shida nyingi,
uchungu na mateso
na vita na misiba
Katika ulimwengu.


4. Kuhangaika kwetu
siku zote ni bure
asipotushikiza 
Yeye atulindaye


5. Na kama mama mwema
anavyomlinda mtoto
katika shida zote,
asipotee njia.


6. Hivyo na Mungu wetu 
hulinda watu wake, 
huwakingia shida, 
huzuni na msiba.


7. Leo atuingiza
    Katika mwaka mpya,
    Hachoki kutupenda,
    Kutufanyia mema.


8. Huruma zako ni mpya
   Kila panapokucha,
   Hizo zinakomesha
  Uchungu wa mioyo.


9. Utabariki sote
Katika njia zetu,
wakubwa kwa adogo
wakalishe mwangani.


10. U Baba wa wakiwa,
u mshauri wa wajinga,
u mponya wa wagonjwa,
u msaada wa maskini.


11. Na Mwisho Twakuomba:
utupe roho wako,
utufundishe hapa,
atuongoze kwako.


12. Wewe mwenye uzima
utupe haya yote
sisi Wakristo wako!
Kwani twakungojea!



 

Comments

Popular posts from this blog

17. Tuimbe na kusifu

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu