44.Mjini Mwake Daudi


1. Mjini mwake Daudi
Bandani mwa mifugo
mtoto alizaliwa
Na mamaye maskini
Mariamu ni mama
Yesu mwanawe mwema.


2. Yesu akawa mbinguni 
    akatoka enzini.
    hakukaribishwa chini
    akalazwa horini.
 akaja kimaskini
  kuketi duniani.


3. Siku za ujana wake
akimheshimu mama
na kumtii katika yote
Kama alivyosema.
Kila mwana na awe 
mtii kama Yeye.


4. Amekuwa hata sasa 
kielelezo chetu
alikuwa na unyonge
kama unyonge wetu
kucheka na kulia 
ni kama sisi sote.


5. Tutamwona waziwazi
ndiyo ahadi yake
sasa aketi mbinguni
katika enzi yake
sote na tumwandame
kwani ni Mfalme wetu.


6. Tutamwona Yeye tena!
Sisi katika kibanda,
Ila juu: na sisi sote,
kwake tutakutana.
Hivyo tutakuwepo
mbele yake daima.



 

Comments

Popular posts from this blog

17. Tuimbe na kusifu

32 Kitoto Mpenzi Lala Wee

143.Mungu ni wa Utukufu